Kikendayan (pia Kisalako) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia na Malaysia inayozungumzwa na Wakendayan kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kikendayan nchini Indonesia imehesabiwa kuwa watu 321,000. Idadi ya wasemaji wa Kikendayan nchini Malaysia ambapo hasa huitwa Kisalako ni 10,700 (2000). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikendayan iko katika kundi la Kimalayiki.